skip to Main Content

MPANDA

Katika kuazimisha kipindi cha mfungo wa kwaresima parokia ya kanisa katoliki Katumba imetoa msaada wa zaidi ya laki saba kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu  kilichopo kata ya nsemlwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Wakizungumza Waumini wa Parokia ya Katumba  wamesema katika mfungo wa kwaresma imewawia vyema  kuguswa na kutoa msaada huo, huku wakiitaka jamii kukitumia kipindi hichi kufanya matendo ya huruma katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Akizungumza kiongozi wa msafara SYLIVESTER GABRIEL amesema wamehamasishana na kuhakikisha wanapata vitu hivyo ili kuendelea kuonyesha upendo kwa jamii kama mafunzo wanayoyapata katika nyumba za ibada hukua akiaja thamani ya vitu hivyovilivyotolewa.

Akizungumza kwa niaba ya mlezi mkuu wa kituo ametoa shukrani kwa parokia kwa kuonyesha upendo kwani yalikuwepo maeneo mengi ambayo vitu hivyo vingetumika, ila imekuwa vyema kuwajali watoto  na kuitaka jamii kuendelea kuwajali watu wenye mahitaji mbalimbali.

Back To Top