Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Dawati la jinsia na watoto Katavi laahidi Kuwalinda wanafunzi ili waweze kutimiza Ndoto Zao.
Katavi
Kitengo cha Dawati la jinsia na watoto Mkoani Katavi Kimewahakikishia Kuwalinda wanafunzi Dhidi ya mienendo Mibovu ili waweze kutimiza Ndoto Zao.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Magamba katika mwendelezo wa kutoa elimu Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia na watoto mkoa wa Katavi Judith Mbukwa amewataka wanafunzi kuepuka makundi yanawapelekea kujiingiza katika makundi ya kiuhalifu, mapenzi katika umri mdogo na kutaka kuzingatia masomo.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Ya Magambawakizungumza kuhusu elimu waliyopatiwa wameahidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa kuhusu matukio ya kiukatili wanayofanyiwa ili waweze kutimiza ndoto zao.
Dawati la Jinsia Tanzania ni kitengo maalumu ndani ya jeshi la polisi kinachoshughulikia kesi na matukio ya ukatili dhidi ya watoto.