Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wanachi kujitokeza kuchangamkia fursa katika kuelekea wiki ya Mwanakatavi.
Na Ben Gadau – Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wanachi kujitokeza kuchangamkia fursa katika kuelekea wiki ya mwanakatavi inayotarajia kuanza Tarehe 25 Oktoba hadi 31 Oktoba.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa Amewataka wananchi kujitokeza ili kuendelea kujifunza katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kilimo,ufugaji na uvuvi.
Aidha Mrindoko amezitaka taasisi za umma,taasisi binafsi na halmashauri kushikiriki kikamilifu kwa kuwaleta wadau katika zoezi hilo la kuadhimisha wiki wa Mwanakatavi.
Katika hatua nyingine Mrindoko ameainisha matukio mbalimbali kuelekea katika wiki ya mwanakatavi yapo matukio mbalimbali ambayo yatafanyika kuanzia October 25 hadi kilele chake ambayo ni October 31,mwaka huu.
Maadhimisho ya wiki ya mwanakatvi kwa mwaka huu 2023 yanakuja na kauli mbiu isemayo ‘’KATAVI YETU TALII,WEKEZA IMARISHA UCHUMI KWA MAENDELEO ENDELEVU NA KAZI IENDELEE’’