skip to Main Content

Ukatili wa kingono,vipigo mila na desturi kandamizi kwa wanawake imeleezwa kuwa tamaduni kandamizi katika Kata ya Mwamkulu na kwa upande wa serikali inaendelea na mipango ya utoaji wa elimu kwa kutumia wataalamu mbali mbali. Picha na John Benjamin

Na John Benjamin-Katavi

Baadhi ya Wananchi katika kata ya Mwamkulu Halmashauri ya Mansiapaa ya Mpanda mkoani  Katavi wametoa maoni mseto kuhusu matukio ya ukatili katika kata hiyo

Wakizungumza katika mdahalo ulioandiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Shidepha Mpanda wamesema kuwa kumekuwepo na matukio ya kikatili kama ndoa za utotoni kwa watoto wenye umri wa 13 kunyanyaswa kwa wanawake kwenye ndoa zao ambapo wameleeza kuwa matukio hayo yanachangiwa na mila na desturi zilizopo katika jamii hiyo.

Mary Biyaro ni Afisa maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani hapa Katavi amesema kuwa katika kata hiyo imekuwa na matukio ya kikatili kama ukatili wa kingono,vipigo na mila na desturi kandamizi kwa wanawake ambapo ameleeza kuwa kwa upande wa serikali inaendelea na mipango ya utoaji wa elimu kwa kutumia wataalamu mbali mbali.

Baadhi ya Wananchi walioshiriki mdahalo huo katika kata ya Mwamkulu wakilisikiza na kuchangia hoja wakati wa mdahalo.

Kwa upande wake Afisa tathimini na ufatiliaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Shidepha Mpanda Marco Kapilipiti amesema kuwa shirika la shidepha limejipanga kutoa elimu kwa jamii kupitia watoa huduma ngazi ya jamii  kuhakikisha mila na desturi zote ambazo zimekuwa zikikinzana na kupelekea kuwepo kwa matukio hayo ya kikatili zinatoweka.

Shirika  la shidepha Mpanda limeandaa mdahalo huo kwa ajili ya kujadili maswala ya ukatili ambayo yamekuwa yakijitokeza katika kata hiyo ya Mwamkulu iliyopo halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani hapa Katavi.

Back To Top