miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
Wananchi wa kijiji cha Magogo kata Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule kijijini hapo.
Na Gladness Richard – Tanganyika
Wananchi wa kijiji cha Magogo kata Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoani hapa wameishukuru serikali kwa kuwajengea shule mpya kijijini hapo.
Wakizungumza na Mpanda radio Fm wananchi hao wamesema kuwa watoto wao walikuwa wanatembea umbali mrefu na hali hiyo iliwafanya wawe na hofu juu ya usalama wa watoto.
Kwa upande wake mkurugenzi wa wilaya ya Tanganyika Shaban Juma amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo mpya utapunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya msingi Kasekese.
Ujenzi huo umeambatana na madarasa sita mapya, vyoo na nyumba moja ya mtumishi huku chanzo cha fedha hiyo kikiwa ni serikali kuu.