skip to Main Content

Vijana wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji ambao wanafanya ramli chonganishi Na wamekuwa wakiwaagiza vijana hao nyeti za wananwake ili wawape njia za mafanikio jambo ambao sio sahihi. Picha na Leah Kamala

Na Leah Kamala-Katavi

Jeshi la polisi mkoani Katavi limewakamata watuhumiwa 115 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu wakiwa na vielelezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema wamewakamata watuhumiwa 17 wakiwa na dawa za kulevya na watuhumiwa 31 wakiwana mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akionyesha baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokamatwa. picha na Leah Kamala

Aidha Wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 27 wakiwa na nyara za Serikali vipande 21 vya wanyama pori na wamefanikiwa kuwapeleka watuhumiwa 29 Mahakamani waliopatikana na hatia na Kuhukumiwa vifungo mbalimbali

Pia kamanda amewaasa Vijana wa kiume ambao hawapendi kufanya kazi na badala yake wamekuwa wakitaka kutafuta pesa kwa njia za mkato ambapo wamekuwa wakienda kwa waganga wa kienyeji ambao wanafanya ramli chonganishi Na wamekuwa wakiwaagiza vijana hao nyeti za wananwake ili wawape njia za mafanikio jambo ambao sio sahihi.

Katika hatua nyingine Jeshi La Polisi Mkoa Wa Katavi Limetoa Wito Kwa Wananchi Kuacha Kujihusisha Na Vitendo Vya Kihalifu Na Wasifiche Taarifa Za Kihalifu Na Wahalifu Hatua Ziweze kuchukuliwa Kwa Wakati.

Back To Top