skip to Main Content

Ndugu hao wameiomba serikali kuhakikisha inatenda haki katika tukio hilo ambalo ni La kikatili na lakusikitisha kwani ni mara yakwanza kutokea katika familia yao” Picha na mtandao

Na Samwel Mbugi-Katavi

Watu watatu wa familia moja wameuawa kikatili na mtu/watu wasiojulikana katika Kijiji cha Bulamata Wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi.

Hayo yamethibitishwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Dkt Mundhiri Bashiri akizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa ni kweli wamepokea miili ya watu watatu wa familia moja, Mama na Watoto wake wawili,  ambao ni Monica Shire (24), Siwema Shija (02) na Yanga Shija mwenye umri wa miezi Nane.

Picha ya Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi Dkt Mundhiri Bashiri akizungumza jinsi walivyopokea miili hiyo.Picha na Anna Milanzi

Kwa upande wao ndugu wa marehem wamesema kuwa walipokea tarifa hizo kutoka kwa mdogo wao akiwaeleza kuwa amekuta familia yake imekatwa mapanga na Mtu /Watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Pia ndugu hao wameiomba serikali kuhakikisha inatenda haki katika tukio hilo ambalo ni La kikatili na lakusikitisha kwani ni mara yakwanza kutokea katika familia yao.

Picha ya Ndugu wa marehem JUMANNE SHIJA akieleza jinsi walivyopokea taarifa hizo. Picha na Anna Milanzi

Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polis mkoa wa Katavi Castar Ngonyani zimefanyika na kusema kuwa upelelezi unaendelea kuhusiana na tukio hilo ambalo limetokea wilaya ya Tanganyika mkoa wa katavi na taarifa rasni itatolewa hivi karibuni.

Back To Top