skip to Main Content

Mpimbwe
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Katavi imetoa elimu ya mabadiliko ya sheria mpya za kodi kwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Mpimbwe pamoja na kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumzia utoaji wa elimu hiyo Meneja wa TRA mkoa wa kodi Katavi Jacob Mtemang’ombe amesema wamepunguza changamoto nyingi zilizokua zikiwakabili wafanyabiashara wa eneo hilo.

Fraseki Mwakalenga ni Afisa Mfawidhi kituo cha kodi Majimoto ambapo amesema kuwepo kwa kituo cha kodi majimoto kumeongeza muamka wa wafanyabiashara kulipa kodi.

Miongoni mwa wafanyabiashara waliofika kupata elimu hiyo Ameomba maafisa wa TRA kufika kufika kwenye biashara kujiridhisha kabla ya kumkadiria mfanyabiashara kodi huku wakishukuru kwa elimu waliyopewa.

Back To Top