Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Katibu mkuu wa Chama Cha mapinduzi taifa Daniel chongolo ameahidi kufanyia kazi mradi wa umeme wa gridi ya taifa
Na John Benjamin – Mpanda
Katibu mkuu wa Chama Cha mapinduzi ccm taifa Daniel chongolo ameahidi kufanyia kazi kuhakikisha mradi wa umeme wa gridi ya taifa unakamilika kwa wakati.
Amebainisha hayo baada ya kuwasili katika mkoa wa Katavi ambapo ameleeza licha ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania daktari Samia Suluhu Hassani kufahamu uwepo wa changamoto hiyo amesema atahakikisha anazungumza na waziri mwenye dhamana kwa ajili ya kuharakisha ukamilikaji wa mradi huo
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mkoa wa Katavi mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa changamoto ya umeme imekuwa kikwanzo kwa upande wa viwanda ambapo Kwa sasa mkoa una kiwanda kikubwa kimoja na hii inatokana na uhaba wa umeme.
Kwa upande mwenye kiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Katavi Iddy Kimanta amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali katika mkoa wa Katavi ila kwa sasa mkoa huo unapitia changamoto ya uhaba wa umeme.