skip to Main Content

Ugonjwa wa macho mekundu mpaka sasa hauna tiba ya  moja kwa moja na huchukua siku mbili hadi tano kuona dalili za ugonjwa huu. “Picha na mtandao

Na Rachel Ezekia-katavi

 Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa macho mekundu  [RED EYES]  Kutokana  na kuathiri watu.

Hayo yamesemwa na daktari wa macho kutoka hospitali ya manispaa ya Mpanda Eckhard Enock  ambapo katika katika ziara ya kutoa elimu  maeneo mbalimbali wamebaini wagonjwa   na   kwa siku huwa wanapokea wagonjwa wa macho mekundu  watatu hadi wanne kutokana na idadi ya wagonjwa.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao na kuonesha kutokuwa na uelewa wa uhakika kuhusiana na ugonjwa  wa macho mekundu.

Kwa mujibu wa  Enock Ugonjwa wa macho mekundu mpaka sasa hauna tiba ya  moja kwa moja na huchukua siku mbili hadi tano kuona dalili za ugonjwa huu.

Back To Top