skip to Main Content

MPANDA
Wajumbe walioshiriki katika baraza la madiwani robo ya mwaka lililofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamemtaka Katibu tawala wa Mkoa kutatua mgororo wa makabidhiano ya hosptali baina ya Manispaa na Mkoa.

Wakizungumza katika baraza hilo baadhi ya wajumbe wamesema kuwa mgororo uliopo ni kutokana na kususasua kwa makabidhiano ya hospitali baina ya Manispaa na Mkoa wa katavi huku wakibainisha kuwa mgorogor huo kwa asilimia kubwa unamuathiri mwananchi ambae ndiye mtumiaji wa huduma hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambae ni Meya wa Manispaa ya Mpanda Hidary Sumry amekiri kuwepo kwa Mgogoro huo huku akiendelea kuuomba uongozi wa Mkoa kupitia kwa katibu Tawala wa mkoa kufanya makabidhiano hayo Mapema ili huduma zianze kutolewa kwa wakati.

Back To Top