Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Wananchi wa mkoa wa Katavi waombwa kuacha kuwapa nguvu na fursa watu wanaodhaniwa kuwa na uwezo wa kufichua wachawi[Kamchape]
Na John Benjamin – Katavi
Wananchi wa mkoa wa Katavi wameombwa kuacha kuwapa nguvu na fursa watu wanaodhaniwa kuwa na uwezo wa kufichua wachawi[Kamchape] ambao wanafanya mambo yanayokiuka sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ambaye ameainisha kuwa ujio wa makundi hayo umehatarisha usalama wa mkoa hususani katika mwambao wa ziwa Tanganyika.
Chongolo amesema kuwa imani za kishirikina ni umasikini na kama jamii inapaswa kujifunza ni kuangalia kwa watu wengi wanaoamini katika ushirikina kwani wanaami kwenye ndoto ambazo kutekelezeka kwake ni ngumu.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Daniel Chongolo yupo kwenye ziara ya siku 6 katika Mkoa wa Katavi ambapo atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na October tatu ametembelea wilaya ya Tanganyika na October 4 anatarajiwa kutembelea wilaya ya Mlele.