skip to Main Content

MPANDA

Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda imefanikiwa kuzirejesha fedha kiasi cha Shilingi Milion moja laki mbili na arobaini na tano zilizochangwa na wananchi wa mtaa wa mtemi beda kata ya misunkumilo ili wapimiwe viwanja.

Akizungumza na Mpanda redio fm Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpanda Keneth Pesambili amesema kuwa mara baada ya kurudishiwa fedha hizo wananchi hao hawaruhusiwi kufanya shughuli zozote za kimaendeleo katika maeneo hayo kama hawana vibali vya ujenzi.

Aidha akishukuru kwa niaba ya wananchi hao Peter Matiampula amesema kuwa dhumuni la pesa hiyo ilikuwa ni kupimiwa viwanja katika eneo ambalo linatajwa kuwa ndani ya bonde huku akiwaasa wananchi kutoendelea na shughuli zozote za maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akiwa katika ziara katika Mtaa wa mtemi beda aliagiza wananchi hao kurejeshewa pesa ambazo zimechangwa na wananchi hao kiasi cha shilingi million 1,245000 (Million moja laki mbili na arobaini na ta

Back To Top