Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemtaka mganga mfawidhi kuhakikisha zoezi la kuhamia hospital mpya ya mkoa kutoathiri utoaji huduma katika hospitali teule ya rufaa.
Mrindoko amesema wahakikishe wanatengeneza miundombinu ambayo yatapelekea wagonjwa kuendelea kutibiwa hospital teule ya rufaa wakati mchakato wa kuhama unaendelea na kuwataka wananchi kutokua na shaka na serikali ya mkoa imejipanga kusimamia mchakato huo.
Dk Seraphine Patrice Mganga Mfawidhi hospital teule ya Mkoa amesema kamati za makabidhiano zimeshaanza kukaa na kuanza makubaliano ili kujua namna bora ya kuhama bila kuathiri utoaji huduma.
Kwa mujibu wa maelekezo ya serikali hospital mpya ya mkoa wa Katavi iliyopo Kazima mkoani hapa inapaswa kuanza kufanya kazi tarehe 14/11/2022.