Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mwamkulu manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamehofia kuharibika kwa zao la mpunga uliopo shambani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa kuna hatari ya kupoteza mazao ya mpunga kutokana na maji kufurika na kujaa kwenye majaruba ya mpunga.
Aidha mkuu wa idara ya kilimo manispaa ya Mpanda Gwalusajo Kapande amesema amewataka wananchi kuondoa hofu kwani hakuna madhara makubwa yatakayo jitokeza, na amewashauri wakulima wa zao la mpunga kulima kwenye maeneo ambayo sio mpito wa mkondo wa maji.
Aidha wakulima pia wametakiwa kutumia njia za kisasa kulima zao la mpunga, ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoweza kujitokeza.