skip to Main Content

MPANDA

Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapa elimu juu ya ugojwa wa surua ambao unasambaa katika kijiji hicho.

Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi wameainisha kuwa baadhi ya familia katika kijiji wanahisiwa kuwa na surua na kuitaka serikali kuwasaidia ili kutokomeza ugonjwa huo.

Aidha Mpanda radio fm imezungumza na mratibu wa chanjo manispaa ya Mpanda Ibrahimu Makidadi na kusema wazazi wanatakiwa kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ili wapate chanjo ya kuwakinga na ugojwa.

Kwaupande wake Mganga mkuu wa manispaa ya Mpanda Dk Paulo Swankala amesema kuwa atatuma watalamu kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii huku akiongeza kuwa watakaobainika na ugojwa watapata chanjo na kutibiwa.

Back To Top