miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…

“Kutokana na shughuli ambazo zimekuwa zikiendelea katika eneo hilo zimekuwa zikiwaathiri kiafya kutokana na kemikali zinazotumika katika kazi hizo sambamba na kelele za mitambo mikubwa iliyopo eneo hilo” Picha na Denis Mkakala
Na Ben Gadau-katavi
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Ikulo kijiji cha Dilifu kata ya Magamba wameitaka kampuni ya uchimbaji ya JEMA kuharakisha kuwalipa fidia ili waweze kuhama maeneo hayo.
Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi wamesema kuwa kutokana na shughuli ambazo zimekuwa zikiendelea katika eneo hilo zimekuwa zikiwaathiri kiafya kutokana na kemikali zinazotumika katika kazi hizo sambamba na kelele za mitambo mikubwa iliyopo eneo hilo.

“Wananchi wanaokumbana na changamoto hiyo walipoketi kujadili kutaka kujua hatima ya kupewa fidia ili wahame maeneo hayo“
Makdonard Julius branch meneja wa Kampuni hiyo ya Jema amesema kuwa kutokana na uhitaji wa maeneo walionao hivi karibuni wataanza kufanya tathmini na utambuzi katika eneo hilo ili wananchi wapate stahiki zao.
Akizungumza kwa njia ya simu Alex Semwali kutoka kitengo cha udhibiti wa mazingira manispaa ya Mpanda amekiri kupokea taarifa za malalamiko ya wananchi juu ya plant hiyo kutumia kemikali zaidi ya moja huku akisema hatua stahiki zinachukuliwa ili kulitafutia ufumbuzi sakata hilo.