skip to Main Content

 ‘Mbunge wa jimbo hilo Anna Lupembe amewataka  wananchi kuendelea kuwa na mshikamano na kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi ili kujikwamua kimaishaPicha na Lilian Vicent

Na Lilian Vicent-katavi

Wananchi wa kata ya Mtapenda wametoa shukrani kwa  Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Halmashauri ya Nsimbo Anna Lupembe kwa kutoa misaada  ikiwemo fedha kwa wajasiliamali.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi walionufaika katika ziara ya kusikiliza kero kwa wananchi wa Jimbo la Nsimbo kata ya Mtapenda  Walipopata nafas kuzungumza na wakizungumza na Mpanda Radio Fm ambapo msaada huo utasaidia kuwakuza kiuchumi.

Akizungumza  Mbunge wa jimbo hilo Anna Lupembe amewataka  wananchi kuendelea kuwa na mshikamano na kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi ili kujikwamua kimaisha.

Ikumbukwe kuwa ziara yake ni Kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi,  kugawa vifaa vya michezo na majiko ya gesi kwa wajasiliamali katika kata zote 12 zilizopo Halmashauri ya Nsimbo.

Back To Top