skip to Main Content

Mwenyekiti wa mtaa wa Mtemi Beda Edisi Kazwika amekiri kupokea tarifa za uwepo wa matukio ya uhalifu katika eneo hilo na kuwahakikishia hatua za usalama zinachukuliwa kwa wananchi wanaopita katika eneo hilo” Picha na mtandao

Na Rachel Ezekia-katavi

Wananchi wa mtaa  wa Mtemi Beda kata ya Minsukumilo Mansipaa ya Mpanda wametakiwa kuchukua tahadhari baada ya  kuibuka uhalifu na uporaji  kwa wananchi wanaopita   maeneo ya karibu na njia inayoelekea  kituo cha Afya cha shule ya sekondari  ya Wasichana  Mpanda Girls.

Akizungumza mtendaji wa mtaa  wa Mtemi Beda  Anipha Mwanangwa amebainisha kupokea kwa taarifa hiyo na wameshafanya kikao cha dharura ili kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo kwa kushirikiana na polisi kata pamoja na wananchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mtemi Beda Edisi Kazwika amekiri kupokea tarifa za uwepo wa matukio ya uhalifu katika eneo hilo na kuwahakikishia hatua za usalama zinachukuliwa kwa wananchi wanaopita katika eneo hilo.

Kwa upande  wake Mhanga aliyenusurika katika moja ya  tukio lililotokea hivi karibuni ameeleza namna ambavyo tukio lilivokuwa  huku mashuhuda na wananchi wa maeneo hayo wameeleza kuwa njia hiyo kwasasa imekuwa sio salama kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Back To Top