skip to Main Content

Ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei  elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaj“.

Na Betord Benjamin-katavi

Jumla ya wafanyabiashara 24 Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi wamekamatwa kutokana na kuuza sukari kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali. 

Akijibu swali la baadhi ya wafanyabiashara  waliohoji juu ya hali ya mwenendo wa bei elekezi ya Sukari Afisa biashara Manispaa ya  Mpanda  Paul Kahoya  amesema ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei  elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji

Akizungumza kwa Niaba ya  Mkuu wa mkoa   wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko  Mkuu wa Wilaya ya  Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wafanyabiashara  Mkoani hapa kufanya shughuli hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni  zilizowekwa na serikali  ikiwa ni pamoja na kulipa kodi.

Kulingana na bei elekezi ya seriksli kilo ya Sukari Mkoani hapa inatakiwa kuuzwa kwa sh 3200 ambapo mfuko wa sukari wa kilo 50 unatakiwa kuuzwa kwa sh 145000

Back To Top