skip to Main Content

KATAVI

Wajasiliamali wadogo wadogo maarufu kama machinga Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamezungumzia changamoto wanazokutana nazo katika utoaji wa mikopo katika vikundi.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm, na kubainisha sababu zinazopelekea baadhi ya vikundi kutopata mikopo baada ya kujisajili , ni kutokana na kutokuwa waaminifu pale wanapopewa mikopo hiyo.  .

.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la machinga Mkoa wa Katavi Marco Ernest, amesema kuwa ni wajibu wa kila kikundi kufuatilia uwezekano wa kupata mikopo baada ya kujisajili, na badala yake wasisubili kufuatwa kwaajili ya kupewa mikopo hiyo.

.

Nae Afisa Maendeleo Mkoani hapa Marietha Mrozi, amesema kuwa wapo tayari kusikiliza  changamoto hizo na kuzitaftia ufumbuzi  hivyo kuwataka wa machinga kufika  ofisini  .

Back To Top