Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI
Mkoa wa Katavi umepokea mradi wa miaka mitano utakao gharimu Bilioni 40 unaosimamiwa na serikali ya Marekani chini ya taasisi ya afya ya Ifakara utakoshirikiana na Mkoa kusimamia huduma za Malaria .
Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo mkurungezi wa mradi kutoka taasisi ya afya Ifakara Dokta Dustani Bishanga amesema mradi huu unalenga kuboresha huduma za malaria kwa kutoa elimu kwa wananchi, kuwaongezea elimu watumishi wa afya pia kuboresha mifumo ya afya.
.
Katibu tawala wa mkoa wa katavi Hassan Abbas Rungwa akizungumza baada ya kupokea mradi amesema mradi huo umekuja kwa wakati sahihi kutokana na hali ya malaria mkoani hapa na kuahidi kutoa ushirikianao katika utendaji na usimamizi .
.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa inayoongoza katika takwimu za malaria nchini hivyo utekelezaji wa mradi wa kuzuia malaria unalenga kupunguza hali ya maambukizi malaria nchini.