skip to Main Content

MPANDA

Hofu ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi imetajwa kuwa ni moja ya sababu kwa baadhi ya wanaume katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kushindwa kuwasindikiza wenza wao kwenye vituo vya kutolea huduma za kilinic pindi wanapokuwa wajawazito.

Hayo yameelezwa na wakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wakati wakizungumza na kituo hiki juu ya uwepo wa badhi ya wanawake wanaolazimika kuwatumia wenzi bandia ili kuwasaidia kufungua kadi ya klinic kwa mjamzito.

Kwaupande wake Mratibu wa huduma za afya ya uzazi amewataka wanawake kutafuta njia nyingine sahihi ili kufungua kadi ya klinic kwa mjamzito badala ya kutumia wenzi bandia ambapo amesema kuendelea kufanya hivyo ni hatari kiafya.

Back To Top