skip to Main Content
Katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo akisalimiana na wenyeji wake mara baada ya kuwasili.

KATAVI
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM taifa Daniel Chongolo Amewasili Mkoani Katavi kuanza Ziara ya Siku 6 kwa ajili ya kukagua miradi na kuzungumza na wananchi.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na chama cha Mapinduzi mkoani Katavi mara baada ya kuwasili amepata nafasi ya kusomewa taarifa maalumu ya chama na serikali ngazi ya mkoa na wilaya.

Aidha katika Siku yake ya Kwanza ya Ziara amepata nafasi ya Kwenda kuhani Msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti Wa chama cha Mapinduzi[CCM] wilaya ya Mpanda Methodi Mtepa aliyefariki mwishoni mwa mwezi wa tisa.

October 3 Chongolo Anatarajiwa kutembelea wilaya ya Tanganyika na kukagua miradi ikiwemo bandari ya Karema, pamoja kufanya mikutano na wananchi kabla ya ya October 4 kuelekea Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.

Back To Top