Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
TRA mkoa wa Katavi imewataka wananchi mkoani hapa ikiwemo wafanyabiashara na wanunuzi kuwa na utaratibu wa kutoa na kudai risiti
KATAVI.
Mamlaka ya mapato mkoa wa Katavi imewataka wananchi mkoani hapa ikiwemo wafanyabiashara na wanunuzi kuwa na utaratibu wa kutoa na kudai risiti ili kuchangia pato la taifa .
Akizungumza na mpanda redio fm kwenye kipindi cha jioni maridhawa meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Katavi Jacobo Mtemang’ombe amesema kuwa ni wajibu wa kila mtu kutoa na kudai risiti baada ya kufanya mauzo na manunuzi huku akitaja faida mbali mbali zitokanazo na kudai risiti ikiwa ni pamoja na kuliingizia pato taifa.
Kwa upande wao baadhi ya wafanya biashara manispaa ya mpanda mkoani katavi wameainisha faida kwa upande wao na kwa serikali mara baada ya kuuza na kutoa risiti kwa mteja anaponunua bidhaa.
Nao baadhi ya wanunuzi wamesema kuwa ni jambo jema kwa wafanyabiashara kutoa risiti kwa mnunuzi ili kutoiingizia serikali hasara kwa kuchangia pato la taifa.