skip to Main Content
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi CCM Taska Restituta Mbogo. Picha na Mtandao

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi kupitia CCM Taska Restituta Mbogo ametoa zaidi ya shilingi milioni tatu kwa ukamilishaji wa ofisi za CCM wilaya ya Mlele na ofisi ya UWT wilayani hapo.

Na Ben Gadau – Mlele
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Katavi kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Taska Restituta Mbogo ametoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya ukamilishaji wa ofisi za CCM wilaya ya Mlele na ofisi ya UWT wilayani hapo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo mbunge amesema kuwa kwa kutambua jitihada zinazofanywa na chama hivyo ameamua kutoa kiasi hicho ili kumalizia ujenzi mapema na kupisha shughuli nyingine za kichama kuendelea.

Joshua Mbwana ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele amemshukuru Mbunge huyo kwa kujitolea kiasi hicho huku akitoa maagizo kwa kamati ya ujenzi wa ofisi hizo kuzitumia fedha hizo kwa weredi na malengo kusudiwa.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe walio jitokeza wamemshukuru Mbunge huyo huku wakisema itakwenda kupunguza changamoto walizokuwa wakikutana nazo hapo awali.

Back To Top