skip to Main Content

Picha na Gladness Richard

zoezi la kusikiliza kero za wananchi ni kwa kila kata ambapo jeshi la polisi litahakikisha linawafikia wananchi wote katika kata hizo

Na Samwel Mbugi -Katavi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani ameanzisha ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kila kata ndani ya mkoa wa Katavi.

Wakieleza kero katika mkutano uliofanyika manispaa ya Mpanda wananchi wameainisha kero ya mabomu wakati wa mazoezi ya jeshi la polisi mkoa wa Katavi ambayo yameonekana kuwakosesha utulivu wananchi kufanya shughuli za maendeleo kero kwa wanaoishi karibu na maeneo wanayofanyia mazoezi

Kamanda wa polisi amethibitisha kuwa ni kweli kunawakati wanaripua mabomu wakati wa mazoezi yao na amewaomba radhi wananchi wanaishi karibu na eneo la jeshi la polis

Hata hivyo kamanda Ngonyani amesema kuwa zoezi hili la kusikiliza kero litakuwa endelevu ambapo atahakikisha anapita kila kata kujua kero za wananchi wa eneo husika.

Back To Top