Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Kukatika kwa umeme baadhi ya maeneo imekuwa inajirudia na kumekuwa hakuna taarifa kutoka mamlaka husika jambo ambalo limekuwa likipeekea changamoto ya kusimama kwa baadhi ya kazi za watu zinazotegemea nishati ya umeme” Picha na Lilian Vicent
Na Lilian Vicent-Katavi
Wananchi wa maeneo mbalimbali mkoani katavi wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kukatika kwa umeme ghafla bila ya kutolewa kwa taarifa kwa umma na TANESCO.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya kashaulili Magret Kitungulu wakati akiuliza swali kufuatia taarifa iliyowasilishwa na TANESCO mkoani hapa katika kikao robo ya tatu cha baraza la madiwani na ameongeza kuwa kukatika kwa umeme baadhi ya maeneo imekuwa inajirudia na kumekuwa hakuna taarifa kutoka mamlaka husika jambo ambalo limekuwa likipeekea changamoto ya kusimama kwa baadhi ya kazi za watu zinazotegemea nishati ya umeme.
Kwa upande wake Afisa masoko mkuu TANESCO Proches Joseph amesema kuwa amepokea suala hilo watajihatihidi kuandaa ratiba itayosaidia watu kufahamu na shughuli zingine ziweze kuendelea.
Nae mstahiki meya Haidary Sumry kwa niaba ya baraza hilo amewasilisha ombi kwa naibu waziri mkuu ambaye waziri wa nishati dotto biteko kuongezewa mashine kwaajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa umeme.
Mstahiki meya Haidary Sumry alipokuwa akiongoza baraza la madiwani. Picha na Lilian Vicent