skip to Main Content

Silaa amesema Kitendo cha kutolipa Kodi ya Pango la Ardhi ndani ya muda uliowekwa na sheria, kinasababisha mmiliki wa ardhi kuvunja moja ya sharti la umiliki” Picha na mtandao

Na John Benjamin-katavi

Baadhi ya wananchi  mkoani hapa Katavi wametoa maoni mseto kuhusu kauli ya waziri wa ardhi wa nyumba na maendeleo  ya makazi Jerry Silaa kuhusu ulipaji wa kodi ya pango na ardhi.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM kwa nyakati tofauti ambapo wamelalamikia kuwepo kwa mlundikano wa kodi hizo, hali ambayo inapelekea kushindwa kulipa kwa wakati na kuiomba mamlaka kupunguza baadhi ya kodi hizo.

Kamishina msaidizi  wa ardhi mkoa wa katavi  Shededi Mrutu ametolea ufanunuzi kuhusu kauli ya waziri wa ardhi Silaa  ambapo ameleeza kuwa  ulipaji wa kodi ya pango la ardhi ni kwa upande wa aridhi iliyopimwa na kumilikishwa ambapo kodi hiyo ni tofauti na kodi ya pango ambayo hutozwa kwa njia ya ulipaji wa umeme.

Waziri wa aridhi wa nyumba na maendeleo  ya makazi Jerry Silaa ametoa siku 30 kuhakikisha wananchi wanalipia kodi ya pango ya aridhi.

Waziri Silaa amesema kuwa kila mmiliki wa ardhi analo jukumu la kulipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka amepewa sharti la kulipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa kila mwaka kwa mujibu wa Fungu la 33 (1) la Sheria ya Ardhi (Sura ya 113).

Waziri amesema kuwa kuwa kwa mujibu wa Fungu la 44 (1) la Sheria ya Ardhi (Sura ya 113), kila mmiliki wa ardhi anatakiwa kutimiza masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na sharti la kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.

Silaa amesema Kitendo cha kutolipa Kodi ya Pango la Ardhi ndani ya muda uliowekwa na sheria, kinasababisha mmiliki wa ardhi kuvunja moja ya sharti la umiliki.

Ameongeza kuwa Wizara kwa nyakati tofauti, imekuwa ikihamasisha na kuwakumbusha wamiliki wa ardhi kulipa Kodi ya Pago la Ardhi. Hata hivyo, baadhi ya wamiliki wa ardhi hawajatekeleza wajibu huo wa kisheria.

Back To Top