Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Mkuu wa mkoa wa katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko alipokuwa akitoa hotuba kwa Wananchi katika viwanja vya kituo cha Afya Nsemulwa katika siku ya familia duniani. Picha na Gladness Richard
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni ‘Tukubali tofauti zetu kwenye familia na tuimalishe malezi ya watoto kwa pamoja kwa kushirikiana Baba,Mama na Wanafamilia wengine’.
Na Gladness Richard-Katavi
Wazazi na walezi mkoani katavi wametakiwa kuwalea watoto wao katika maadili mema ili kuhakikisha wanajenga familia iliyo bora.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko wakati alipokuwa akitoa hotuba yake kwa Wananchi wa mkoa wa katavi katika siku ya familia duniani huku akiwataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao katika maadili mema.
Kwa upande wao Wananchi walioudhuria maadhimisho hayo wamesema kuwa Wazazi kutokuzungumza na watoto wao kunasababisha mmomonyoko wa maadili kwenye familia.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza na kufuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa katavi katika viwanja vya kituo cha Afya Nsemulwa katika siku ya familia duniani.
Siku ya familia duniani huadhimishwa kila ifikapo mei 15 kila mwaka na mwaka huu katika mkoa wa katavi imeadhimishwa katika kituo cha Afya cha Nsemulwa katika kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda huku ikiambatana na kauli mbiu isemayo ‘Tukubali tofauti zetu kwenye familia na tuimalishe malezi ya watoto kwa pamoja kwa kushirikiana Baba,Mama na Wanafamilia wengine’