skip to Main Content
This image has an empty alt attribute; its file name is ffff-1024x634.jpg

Huenda ametugeuka kwakuwa eneo lake limeachwa wazi hivyo tunazani kuwa zipo sababu za yeyeye kuegemea upande mmoja na kusababisha maeneo hayo kuchukuliwa na jeshiAlisema mmoja wa wananchi aliehudhuria kliniki hiyo. Picha na lilian VIcent

Na lilian VIcent-katavi

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameendelea  na kliniki ya kusikiliza kero  ambapo  kumeibuka hoja ya mgogoro  wa muda mrefu wa  mipaka kati ya  Jeshi La Wananchi Tanzania      [JWTZ ] na Wananchi wa  halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Hayo yamejiri katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda ambapo mmoja  wa Wananchi amesema kuwa kiongozi wao waliomchagau  kusimamia mgogoro huo huenda amewageuka kwakuwa eneo lake limeachwa wazi hivyo wanazani kuwa zipo sababu za yeyeye kuegemea upande mmoja na kusababisha maeneo hayo kuchukuliwa na Jeshi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Mwanamvua Hoza  Mrindoko amebainisha  kwa taarifa aliyonayo mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu  tayari umemalizika kwa mujibu wa wataalamu  na Wanachi wameshiriki na endapo kuna upande au mtu  hajaridhishwa  na uamuzi huo aende mahakamani.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amezitaka ngazi zote kuanzia kwa Katibu Tawala Mkoa, halmashauri zote, wakuu wa taasisi na vyombo vya dola kushughulikia kero zote bila kusubiri siku maalum ya kusikiliza kero.

This image has an empty alt attribute; its file name is pppppp-1024x636.jpg
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza  Mrindoko alipokuwa akizungumza kuwa taarifa alionayo ni kuwa mgogoro huo umamalizika. Picha na Lilian Vicent

Pia baadhi ya wananchi wamelalamikia baadhi ya viongozi katika ofisi kuwa na tabia ya ubinafsi katika ofisi za umma, ambao Mwanachi mwingine amemwambia Mkuu wa Mkoa kuwa baadhi ya Watumishi wa Umma wanakwamisha mambo kwa makusudi kwani badala ya kusikiliza na kutatua kero za wanachi wamekuwa na tabia ya ‘Umungu Mtu’ kitendo alichokitaja kama kuigombanisha Serikali na wananchi.

Back To Top