skip to Main Content

MPANDA

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni yao jinsi mama aliye na maambukizi ya virusi vya ukimwi anavyoweza kumlinda mwanae asipate maambukizi hayo.

Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wamesema kuwa mama anatakiwa kwenda kwenye kituo cha huduma za afya ili kuwahi mtoto asipate maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Kwa upande wake mratibu wa huduma ya ukimwi mkoa kutoka ofisi ya mganga mkuu Solomoni Samweli amesema kuwa kama mkoa kuna huduma wanayotoa ili mama asimwambukize mtoto virusi hivyo.

Solomoni ameongezea kwa kusema mwanamke mjamzito ambaye ana virusi vya ukimwi anasaidiwa kwa ukaribu pindi anapojifungua ili asiweze kumwambukiza mtoto.

Back To Top