skip to Main Content

KATAVI

Wakulima wa zao la Pamba kijiji cha vikonge kata ya Tongwe Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kupitia Wizara ya kilimo kuongeza bei ya zao hilo.

Wakizungumza katika uzinduzi wa soko la Mauzo ya zao la Pamba katika kijiji cha vikonge wananchi hao wamesema changamoto ya kubadilika kwa bei imekuwa ikishindwa kuwanufaisha wakulima katika msimu wa mavuno.

Dorashaz Venance ni mwenyekiti wa chama kikuu cha LATCU amewataka wananchi kulima kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea ili kupata faida ya zao hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi kuwa watulivu huku akiendelea kuwaasa wakala wa ununuzi wa zao la Pamba kuwa na weredi na kuepuka kumnyonya mkulima wakati wa upimaji na uuzaji wa zao hilo.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayakilimo

#bodiyapamba

Back To Top