skip to Main Content

MPANDA

Katibu tawala wa mkoa wa Katavi Hassan Rugwa Amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani hapa kuhakikisha wanatenga bajeti ili kuwezesha sekta ya michezo.

Akizungumza wakati wa Kufungwa kwa mashindano ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi Tanzania [UMITASHUMTA ] amesema kukosekana kwa usimazi dhabiti kunafanya kukosa msukumo na kuwataka kuweka kipaumbele kwenye sekta ya michezo.

Katika hatua nyingine Rugwa amewataka wakurugenzi kusimamia vyema vipindi vya michezo mashuleni na wakuu wa shule kuhakikisha maeneno ya shule yanapimwa ili kuepusha kubadilishiwa matumizi kwa viwanja vya michezo.

Awali Akisoma taarifa ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za shule za msingi Tanzania [UMITASHUMTA ] kwa mwaka 2023/2024 afisa michezo wa mkoa wa Katavi Karoli Steven amesema jumla ya wanamichezo 385 wameshiriki michezo mbalimbali kutoka halmshauri mbalimbali ili kuwapata wataowakilisha mkoa wa Katavi katika mshindano ya Kimataifa.

Michezo ya Umitashumta kitaifa Inatarajiwa kuzinduliwa mkoani Tabora june 04 na makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr Isdory Mpango huku kauli mbiu ni michezo sanaa na taaluma kwa maendeleo ya uchumi na viwanda.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayasanaautamaduninamichezo

#wizarayatamisemi

Back To Top