Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewataka wazazi na walezi kuzingatia mahitaji muhimu ya Watoto .
Na Ben Gadau – Katavi
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewataka wazazi na walezi kuwatimizia mahitaji muhimu Watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi ya kihalifu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha kumekucha Tanzania ambapo amesema baadhi ya Watoto wamekuwa wakijiingiza katika makundi ya kihalifu kutokana na kushindwa kutimiziwa mahitaji maalumu.
Aidha Ngonyani ameendelea kuiasa jamii kwa kushirikiana na wenyeviti wa vijiji na mitaa kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni Pamoja na kutoa taarifa za matukio ya kihalifu.