skip to Main Content
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akizungumza na watendaji.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaonya watendaji wa zembe katika ngazi ya Kata,Mitaa na Maafisa Tarafa

Na Bertold Chove – Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaonya watendaji wa zembe katika ngazi ya Kata,Mitaa na Maafisa Tarafa kufanya Kazi Kwa uwajibikaji kutatua kero za Wananchi kwenye maeneo wanayoyasimamia.

Watendaji wa mitaa na Kata pamoja na Maafisa Tarafa wamekuwa mboni ya serikali katika ngazi ya Kata Kwa kuwahudumia wananchi kwa vitendo kwa kutatua kero za wananchi.

Mrindoko ameyasema hayo alipokutana na watendaji katika kikao Kazi Cha kukumbushana wajibu na Majukumu ya Kila siku katika kuisadia  serikali kiutendaji.

Amesema kuwa watendaji wa mitaa na Kata pamoja na Maafisa Tarafa wamekuwa mboni ya serikali katika ngazi ya Kata Kwa kuwahudumia wananchi kwa vitendo kwa kutatua kero za wananchi.

Baadhi ya watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi

Kuhusu miradi ya maendeleo amewaagiza watendaji hao kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao na kuisemea Kwa wananchi juu ya umuhimu wa miradi hiyo Kwa wananchi kwenye maeneo yao.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kwenda kusimamia ulinzi na usalama kwenye Kata zao kwa vitendo Ili kudhibiti matendo ya uhalifu yanayojitokeza kwenye baadhi ya Mitaa na Kata.

Back To Top