Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Wananchi wa kitongoji cha Ivungwe B kata ya kasokola wameuomba uongozi wa kata hiyo kumaliza migogoro baina ya wafugaji na wakulima
Na Ben Gadau – Mpanda
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Ivungwe B kata ya kasokola wameuomba uongozi wa kata hiyo kumaliza migogoro baina ya wafugaji na wakulima wa eneo hilo.
Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi hao wamesema wamekuwa wakikumbana na changamoto ya baadhi ya wafugaji kulisha mazao katika mashamba ya wakulima hali ambayo inapelekea sintofahamu kwa wakulima hao.
Clisant Mwanawima ni diwani wa kata ya Kasokola akizungumza kwa njia ya simu na Mpanda Redio FM amesema serikali ya kata hiyo imeagiza wataalamu kupima maeneo yanayo milikiwa na wafugaji hao ili kujua chanzo cha migogoro hiyo huku akisema kata hiyo haina maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya wafugaji.