Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
“Jeshi la zimamoto lililoundwa kwa sheria namba 14 ya mwaka 2007 jukumu lake kubwa ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto ,mafuriko ,teteeko la ardhi ,ajali za barabarani pamoja na majanga mengine” Picha na Mtandao
Na Lilian Vicent-katavi
Wananchi wa mtaa wa Mnazi mmoja kata ya Uwanja wa ndege Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamepewa Elimu kuhusu hatua za kuchukua tukio la moto linapotokea na vizimia moto vinavyotumika kulingana na madaraja ya moto.
Afisa habari wa zimamoto mkoani hapa Catherine Sambagi wakati akitoa Elimu amewataka Wananchi kutambua aina mbalimbali za moto ili kupunguza athari zitokanazo na kutumia vizimia moto tofauti kulingana na aina ya moto.
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa mtaa huo wamewashukuru jeshi la Zimamoto kwa kufika na kutoa na elimu kwani itasaidia kupunguza majanga yamoto na wamewakata mamlaka zingine kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa jamii.
Elimu hiyo inayotolewa katika maeneo mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ni katika kutekeleza majukumu ya Jeshi la zimamoto lililoundwa kwa sheria namba 14 ya mwaka 2007 huku jukumu lake kubwa ni kuzima moto na kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto ,mafuriko ,teteeko la ardhi ,ajali za barabarani pamoja na majanga mengine.