skip to Main Content

KATAVI

Madereva wa vyombo vya moto mkoa wa Katavi wametakiwa kutumia muda ulioongezwa kuhakiki leseni zao ili kuepusha usumbufu unaowezajitokeza kwa kutohakiki leseni zao.

Kauli hiyo imetolewa na askari kutoka kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi Geofrey Brighton amesema kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Katavi linafanya ukaguzi wa leseni wa hiari hivyo madereva wanapaswa kupeleka leseni zao ili zihakikiwe.

Kwa upande wao baadhi ya madereva wa vyombo vya moto mkoani hapa wamekiri kuwa upo umuhimu wa dereva kuwa na vyeti vya kazi yao ikiwa ni pamoja na leseni.

Zoezi hilo la uhakiki wa leseni limeanza mwezi march mwaka huu bado linaendelea.

Back To Top