miongoni mwa Takataka ambazo zipo katika maeneo ya makazi ya watu mtaa wa Mpadeco.picha na…
MPANDA
Asilimia 88 ya kaya katika manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatumia vyoo bora huku asilimia 12 za kaya zilizobaki hazina vyoo bora kutokana na kuwa na hali duni ya Maisha.
Akizungumza na Mpanda radio FM afisa afya Manispaa ya Mpanda Erick Kisaka amesema kutokana na kampeni zinazofanywa za kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora ambapo mafanikio yameonekana.
Aidha Kisaka ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyopo zipo kaya ambazo hazina choo kabisa , kutokana na hali duni ya maisha ambapo ameishauri jamii kushirikiana na kusaidia kaya hizo ili ziweze kuwa na choo bora na kuondokana na uharibifu wa mazingira.
Kisaka amesema kwa wananchi ambao wanatiririsha maji machafu ikiwamo ya choo katika maeneo yao hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinahatarisha usalama wa wakazi husika katika maeneo hayo.