skip to Main Content
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu katika kikao na wananchi wa Kagunga.

Wazazi na walezi wa Kagunga kata ya Kasekese wilayani Tanganyika wameshauriwa kuunda kamati ya chakula.

Na Gladness Richard – Tanganyika
Wazazi na walezi wa kijiji cha Kagunga kata ya Kasekese wilayani Tanganyika mkoani Katavi wameshauriwa kuunda kamati ya chakula kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo 2024.

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Tanganyika,Onesmo Busweru wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye shule mpya ya sekondari Kagunga ambapo amesema kuwa wanafunzi waanze kupata chakula shuleni ifikapo mwaka 2024.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wameishukuru serikali kwa kuleta ujenzi wa shule eneo hilo kwani utatatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta elimu.

Zaidi wa milioni 600.38 umetumika kujengea shule mpya ya sekondari ya kagunga huku chanzo cha fedha hiyo ni serikali kuu.

Back To Top