Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
10 October 2023, 12:15 pm
Waumini wa Madhehebu mbalimbali Mkoani Katavi wameombwa kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee kwa kuwapa msaada wa mahitaji ya kiubinadamu
Na Veronica Mabwile – Mpanda
Waumini wa Madhehebu mbalimbali Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameombwa kuwapa kipaumbele watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee kwa kuwapa msaada wa mahitaji ya kiubinadamu ikiwemo chakula ili kuwawezesha kuyamudu maisha
Wito huo umetolewa na Makamu Mkuu Askofu wa kanisa la PENTEKOST CHIRISTIAN CHURCH TANZANIA [PCCT] Steveni Nyanzira wakati wa zoezi la ugawaji wa chakula kwa wahitaji lilofanyika katika kanisa hilo lilopo mtaa wa Mnazi mmoja kata ya Uwanja wa Ndege na kusema kuwa ili kuwasaidia kuwaondolea msongo wa Mawazo.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazi mmoja Arufani Buteme akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi diwani wa kata ya uwanja wa ndege Maiko Kamande amelishukuru Kanisa hilo na kuiomba jamii kuishi maisha ya kusaidiana.
Wanufaika wa msaada huo wamesema kuwa wamekuwa wakitengwa na jamii kutokana na mitazamo tofauti tofauti ikiwemo jamii kuwachukulia kuwa watu wasio sitaili kusaidiwan jambo ambalo lina wafanya kuishi maisha ya dhiki sana