Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Wananchi Mkoani Katavi waliomba jeshi la zima moto na uokoaji kutoa elimu ya vifaa vya kuzimia moto
Na Lusy Dashud -Mpanda
Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameomba jeshi la zima moto na uokoaji kutoa elimu zaidi juu ya matumizi ya vifaa vya kuzimia moto
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti na kuongeza kuwa wengi wao hawana uelewa wa kutosha na fire hydrant (visima vya kuzimia moto) huku wengi wao wakiichanganya na Fire Extinguisher.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Jeshi la Zima moto mkoa wa katavi Coplo Paul Mtani Masungwa amesema kuwa ni muhimu kuwa na visima hivyo vya kuzimia moto (fire hydraaant) kwani vinarahisisha kazi na kuwa haviwezi kutumika na raia wa kawaida isipokua maafisa wa jeshi la zimamoto.
Coplo Masungwa ametoa rai kwa wananchi kutoa msaada kwa mtu mwenye changamoto inayohitaji msaada wa haraka kuliko kuacha hadi wao wafike hali ambayo wakati mwingine uleta maafa zaidi.