skip to Main Content

Wananchi Katavi washauriwa kumaliza dozi za dawa wanazoandikiwa

Na Kalala Robert – Mpanda
Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameshauriwa kumaliza dozi za dawa wanazoandikiwa na madaktari ili kuweza kuuwa vijidudu na kuacha afya zao zikiwa salama.

Mtu asipomaliza dozi ya dawa alizopewa na daktari anaweza kujisababishia ugonjwa kujirudia

Ushauri huo umetolewa na Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Town clinic dokta Gabriel Elias wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm na kusema kuwa mtu asipomaliza dozi ya dawa alizopewa na daktari anaweza kujisababishia ugonjwa kujirudia huku akiwataka wananchi watumie dozi sahihi waliyopangiwa.

Wananchi mkoani hapa wameeleza madhara wanayoyafahamu kutokana na mgonjwa kutomaliza dozi ya dawa aliyopatiwa.

Back To Top