Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
Wanananchi wa kijiji Cha Ikolongo Halmashauri ya nsimbo mkoani katavi wameomba wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu ushiriki wa wanaume kwenda kliniki.
Na Festo Kinyogoto – Nsimbo
Wanananchi wa kijiji Cha Ikolongo Halmashauri ya nsimbo mkoani katavi wameomba wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu ushiriki wa wanaume kwenda kliniki wakati wa ujauzito ili kiwasaidia maandalizi ya kujifungua.
Wamesema hayo wakatiki wa tukio la uhamasihaji kuhusu taarifa potofu katika jamii kuhusu baadhi ya magonjwa ambapo wamesema wanaume wengi wamekuwa wagumu kuhusu ushiriki kwenda kliniki ili kupata elimu kwaajili ya kuandaa vifaa vya mwanamke kujifungua pamoja na kumkinga mtoto atakaezaliwa dhidi ya maladhi ambayo yanawesa kuepukika.
Akijibia hoja hiyo Mganga mfawidhi wa zahanati ya Kijiji Cha ikolongo Ramadhani Abdallah Mshana amesema wanajitahidi kuendelea kutoa elimu Kwa wanaume kushirikiana na wake zao kuanzia hatua ya kwanza ya ujauzito hadi wakati wa kujifungua ili kumlinda mama pamoja na mtoto.
Katika hatua nyingie mganga amesema taarifa za kuanda vifaa kwaajili ya kujifungua zimekuwa zikitolewa ili kuwapa utayari wasipate changamoto pindi inapofika wakati wa kujifungua.
Katika tukio Hilo dhana mbalimbali kuhusu magonjwa zilitolewa ufafanuzi ili kuiweka jamii katika muono chanya kuhusu imani potofu ambazo zimekuwa zikiathiri jamii kutokana na kutopata elimu ya kutosha kuhusu afya.