Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
KATAVI.
Vijana Mkoani katavi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambalage Nyerere kwa kuwa wazarendo na kudumisha amani ya taifa kuelekea kumbukizi ya miaka 23 ya kifo chake.
Kauli hiyo imetolewa na Rafael Peleleza kijana ambae anamuenzi baba wa taifa kwa kufanya matembeTi ya twende Butiama kwa usafiri wa baiskeli kutoka mkoani hapa .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amempongeza Rafael kwa kufanya kitendo cha kishujaa huku akiwataka vijana wengine kuiga mfano huo wa kumuenzi baba wa taifa kwa kujitoa kwaajili ya maslahi ya Taifa.
Matembezi ya kumbukizi ya kumuenzi hayati baba wa taifa yanafanyika kila tarehe 2 ya mwezi octoba huku kilele chake ikiwa ni tarehe 14 mwezi octoba kila mwaka.