skip to Main Content

Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa maji Juma Aweso kuhakikisha anafika kata za Karema na Ikola Kutatua changamoto ya maji

Na John Benjamin – Tanganyika
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi taifa Daniel Chongolo amemtaka Waziri wa maji Juma Aweso kuhakikisha anafika kata za Karema na Ikola Kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa maeneo hayo.

Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa Chama Cha mapinduzi taifa Daniel Chongolo baada ya meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Katavi kushindwa kujieleza ambapo Chongolo amesema kuwa ifike muda serikali inapaswa kuhakikisha wananchi wanapata Huduma ya maji safi.

Meneja wa maji safi na usafi wa mazingira mkoani Katavi Ruwasa Peter Ngunula amesema kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata Huduma ya maji safi na salama kwa asilimia mia moja ambayo yanasukumwa kutoka chanzo kilichopo Karema kwa nishati ya umeme wa Sola.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Sulemani Kakoso amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo katika maeneo hayo ambapo amesema serikali imetenga bilioni 6 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maji katika maeneo mbali mbali ndani ya wilaya Tanganyika.

Back To Top