Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
NSIMBO
Wakulima wa zao la Tumbaku halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wameutaka uongozi wa kampuni ya ununuaji wa Tumbaku ya Mkwawa kuharakisha kufanya malipo ya zao hilo.
Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti wakulima hao wametaja kuwa ucheleweshwaji wa malipo ya zao hilo imekuwa adha kwao huku wakisema wamekuwa wakishindwa kutekelza baadhi ya shughuli za kimaendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Nsimbo AMCOS Cledo Alcado Kasokola amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya kuchelewa kwa malipo huku pia akiendelea kuwataka wakulima hao kuwa wavumilivu wakati wakiendelea kufatilia hatma ya malipo hayo.