Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
MPANDA
Wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda wamesisitizwa kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao.
Msisitizo huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ziwa Tanganyika (Rukwa/Katavi) Ambele Mwaipopo wakati wa zoezi la kugawa taulo za kike kwa wanafunzi hao zoezi lililoandaliwa na Idara ya wanawake KKKT Jimbo la Katavi amesema ili kufikia mafanikio hawanabudi kusoma kwa bidii.
Mwenyekiti wa Idara ya wanawake KKKT Jimbo la Katavi Felista Chaula amesema kama wanawake Jimbo la Katavi wameona haja ya kutoa msaada wa taulo za kike kwa wasichana hao.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Nyabise Sabasi ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na Idara hiyo ya wanawake.
Nao baadhi ya wanafunzi wakatoa shukrani kwa kupatiwa taulo hizo zitakazo wasaidia kujisitili wakiwa katika masomo.