Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA akizungumza KATAVI Mwenyekiti wa chama cha demokrasia…
DAR ES SALAAM
Ikiwa zimepita siku 15 tangu Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) kutangaza mgao wa maji, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema hali bado si shwari.
Aweso ametoa kauli hiyo leo alipotembelea mradi wa visima saba vya Kimbiji ambao unatarajiwa kumaliza changamoto ya maji katika wilaya ya Kigamboni.
Waziri huyo ameeleza kuwa licha ya jitihada zinazoendelea kufanyika kwa kuwaondoa wanaochepusha maji kwenye mto Ruvu bado maji yanayoshuka si kama ilivyokuwa hapo awali hivyo amewataka wakazi wa jiji hilo kuwa na matumizi mazuri ya maji yanayopatikana.